Home » » MKUU WA MKOA WA MOROGORO MH, JOEL BENDERA NA NAIBU WAZIRI WA ARDHI,NYUMBA NA MAENDELEO YA KAZI DR.JOEL OLE MEDEYE WATUNUKIWA PhD ZA HESHIMA

MKUU WA MKOA WA MOROGORO MH, JOEL BENDERA NA NAIBU WAZIRI WA ARDHI,NYUMBA NA MAENDELEO YA KAZI DR.JOEL OLE MEDEYE WATUNUKIWA PhD ZA HESHIMA




Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera ( kushoto) akipongezwa na Makamu wa Rais na Mkurugenzi wa Mahusiano wa Masuala yote ya Afrika ya Kielimu ambaye pia ni Kamishina wa Tume ya Haki za Binadamu yenye kutetea matatizo ya Haki za Binadamu Kimataifa , Profesa Edward Lazaro Nasioki, ( kulia) mara baada ya kumtunukisha Shahada ya Uzamivu ya Heshima ( PhD) katika Masuala ya Falsafa ya Jamii ya Chuo Kikuu cha Califonia State Christian kilichopo nchini Marekani, kwa mamlaka aliyopewa na Bodi cha Chuo Kikuu hicho.


Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera akivishwa kofia ya udaktari wa Heshima .


Naibu Waziri wa Ardhi , Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Dk Joel Goodluck Ole Medeye ( kushoto) akipongezwa na Makamu wa Rais na Mkurugenzi wa Mahusiano wa Masuala yote ya Afrika ya Kielimu ambaye pia ni Kamishina wa Tume ya Haki za Binadamu yenye kutetea matatizo ya Haki za Binadamu Kimataifa , Profesa Edward Lazaro Nasioki, ( kulia).kati kati kati ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Morogoro, Innocent Kalongeris.


Naibu Waziri wa Ardhi , Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Joel Goodluck Ole Medeye ( kushoto) , na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera ( kulia ) wakiwa katika picha ya pamoja na na Makamu wa Rais na Mkurugenzi wa Mahusiano wa Masuala yote ya Afrika ya Kielimu ambaye pia ni Kamishina wa Tume ya Haki za Binadamu yenye kutetea matatizo ya Haki za Binadamu Kimataifa , Profesa Edward Lazaro Nasioki, wa Chuo Kikuu cha Califonia State Christian kilichopo nchini Marekani, baada ya kuwatunukishaShahada ya Uzamivu ya Heshima ( PhD) katika Masuala ya Falsafa ya Jamii ,Novemba 30, mwaka huu kutokana na mamlaka aliyopewa na Bodi cha Chuo Kikuu hicho.Picha na John Nditi, Morogoro



Na John Nditi, Morogoro



MKUU wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera , na Naibu Waziri wa Ardhi , Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Joel Goodluck Ole Madeye , wametunukiwa Shahada ya Uzamivu ya Heshima katika Masuala ya Falsafa ya Jamii ya Chuo Kikuu cha Califonia State Christian kilichopo  nchini Marekani.



Bendera na Medeye walitunukishwa PhD zao ,Novemba  30, mwaka huu  na Makamu wa Rais na Mkurugenzi wa Mahusiano wa Masuala  yote ya  Afrika ya Kielimu ambaye pia ni Kamishina wa Tume ya Haki za Binadamu yenye kutetea matatizo ya Haki  za Binadamu Kimataifa , Profesa Edward Lazaro Nasioki, kwa mujibu wa  mamlaka aliyopewa na Bodi cha Chuo Kikuu hicho.



Kabla ya kuwatunukisha , Profesa Nasioki , alisema moja ya kazi za Vyuo Vikuu Duniani ni kwenda katika jamii kutafuta watu walionasifa mbalimbali , waliobuni na kuchangia maendeleo ya aina mbalimbali katika jamii.



Alisema , PhD hutolewa hasa kwa watu wale waliotumia muda wao kwa miaka mingi kusoma , kufanya utafiti wa mambo mbalimbali katika jamii au kiroho na kupendekeza au kushauri juu ya njia za kuleta mabadiliko yenye manufaa kwa jamii na hao wanatambuliwa kama wataalamu mbalimbali wahusika.



Hivyo alisema , Shahada ya heshima hutolewa hasa kwa wale watu ambao wamatumikia muda na rasilimali zao kubuni na kuchangia michango ili kutatua matatizo yanayoikumba jamii ,hivyo Chuo hicho kimetambua juhudi , elimu , maisha , tabia , utendaji na mchango wa Bendera na Medeye katika jamii ya Tanzania .



“ Tuko hapa leo , Nov emba 30 , mwaka huu kwa ajili ya kutunuku shahada ya heshima kutokana na historiana mchango wenu kwa jamii ya Watanzania” alisema Profesa Nasioki ambaye ni Mtanzania mbele ya wageni waalikwa walihudhuria hafla hiyo katika viwanja vya Ikulu Ndogo ya Mkoani Morogoro.



Kwa mujibu wa Makamu wa Rais wa Chuo hicho,Watanzania 117 wamepata shahada za aina mbalimbali kutoka Vyuo vya Marekani , Canada na Korea , kati ya hao watatu wamepata shahada za heshima na tisa shahada za uzamili.



Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Bendera, akizungumza baada ya kutunukiwa PhD, aliishukuru Bodi ya Chuo Kikuu hicho kwa  kutambua mchango wake katika taifa na kuweza kumtunukia Udaktari wa Heshima.



 Hivyo alisema  , kupata PhD ni chachu na changamoto kwake  ya kuwatetea mabadiriko ya kimaendeleo mara mbili zaidi ya utendaji kazi kwa Watanzania wakiwemo na  wananchi wa Mkoa huo.



“ Mtu asifirikie kutunukiwa PhD sasa nitakweteka la hasha , hii ni changamoto na kipimo kingine cha kuendeleza kazi ya maendeleo ya wananchi kwa kushirikiana na watendaji wengine wa Wilaya na mkoa “ alisema Dk Bendera.



Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Medeye ,alisema , Chuo Kikuu hicho kimetambua uwezo wao na sifa zao , hivyo  kazi iliyopo mbele ndani ya  Wizara kwa kushirikiana na watendaji wengine ni kujituma kwa bidii na utendaji unaozintatia haki ,taratibu na sheria.
KWA HISANI YA MICHUZI BLOG



0 comments:

 
Supported by : Tone Media
Copyright © 2012. Morogoro Yetu - All Rights Reserved
Template Modify by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa